Manfongo Achukizwa na Sungusungu .

Msanii wa  muziki wa kisingeli nchii, Manfongo amesema kuwa amekatishwa tamaa sana na ufanyaji kazi wa sungusungu kutokana na kubambikiwa kesi kwa baadhi ya wananchi bila kuwa na makosa yoyote.

Manfongo ameongea hayo alipokuwa akiongea na eNews huku ikiwa imepita siku chache tu tangu aliporipotiwa na baba yake mzazi kuwa msanii huyo aliwekwa ndani kutokana na kosa la kukutwa na bangi.

download latest music    

Sungusungu wa  Ali Maua wamekuwa na tabia mbaya sana wamekuwa wakifanya kazi knyume na utaratibu sana naomba waondolewe tubaki na polisi kama kuna tatizo tutaenda kusema polis tu maana wale sungusungu wanasumbua vijana pamoja na wananchi na wakina mama sana.

Kitu kikubwa alichosema manfongo ni kuwa sungusungu wamekuwa na tabia ya kuomba pesa kila wanapokutana na raia na kama unakuwa una pesa hiyo basi inakuwa kama umefanya kosa na kukamatwa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.