Mange Kimambi: Diamond Ndio Alimuacha Zari

Tangu jana stori kubwa inayotawala kwenye mitandao ya kijamii ni kuvunjika kwa mahusiano ya Supastaa wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na mama watoto wake Mfanyabiashara Zari The Bosslady.

Siku ya Wapendanao Zari alitumia ukurasa wake wa Instagram kujulisha mashabiki zake kuwa yeye na Diamond wameachana lakini kikubwa zaidi alichoweka wazi Zari ni kuwa sio tu yeye na Diamond hawako wote bali yeye ndio amemwacha Diamond sababu ya kuchepuka ambapo aliandika:

download latest music    

There have been multiple rumors some with evidence floating around in all sorts of media in regards to Diamond constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond..”.

Zari amejaribu kuweka wazi ijulikane wazi kabisa na  umma kuwa yeye ndio aliyemuacha Diamond kitu ambacho Mange ameibuka na kudai kuwa sio kweli na kudai Diamond ndio alikuwa wa kwanza kumuacha Zari kwa sababu alikuwa ameshamchoka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika maneno haya akimtuhumu Zari kwa kudanganya:

No no no honey, you didn’t leave Diamond, Diamond ndio alikuacha, mara ngapi Dogo alikuwa anakuonyesha kuwa hakutaki wewe ndio ulikuwa unamng’ang’ania? Ulivhotakiwa kusema leo ni kwamba umekubaliana na hali halisi kuwa dogo hatokaa kutulia kwa ajili yako. Wewe usituchezee akili eti umemuacha. Nyambaafu ulijua kuzaa fasta ndio kumkamata mwanaume! Umenyooooshwa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.