Loading...

Maoni ya Dogo Janja kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize

May 18, 2017 at 14:47
Maoni ya Dogo Janja kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo Janja ametoa maoni yake kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize kufuati matukio ya hivi karubuni.

Kuliibuka uvumi kuwa wawili hao (Harmonize na Wolper) waliachana lakini baadae Harmonize alikuja kuthibitisha ukweli wa mambo.

Dogo Janja alikuwa na mengi ya kusema kuhusu uhusiano wa Wolper na Harmonize; akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, msanii huyo wa Tip Top Connection inayomilikiwa na Babu Tale, alisema kuwa maisha ya watu mashuuri ni filamu.

Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo alisema kuwa mapenzi ya Harmonize na Wolper ulikuwa kama drama ulipokua unaanza lakini mwishowe ukawa ‘serious’.

“Ukishakuwa na mpenzi staa hiyo ni flamu tayari, maisha yenu ni filamu watu wanafuatilia. Kingine mapenzi yao yalivyokuwa yananza watu walikuwa wanachukulia kama Drama lakini mwisho wa siku unakuja kuona kama wapo serious, kwa hiyo ni vitu kama hivyo.

“Mimi kama mimi siko interested nao sana, ni verse tu zile, siko interest nao kwa vile na mimi nina mapenzi yangu , kila mtu ana mitikasi yake” amesema Dogo Janja.

Dogo Janja

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere