Loading...

Maoni ya wasanii Kuhusu Adhabu kwa Wanaume Kukohoa Wanapopita Wanawake Wenye Maumbo Makubwa

May 16, 2018 at 10:50
Maoni ya  wasanii  Kuhusu Adhabu kwa Wanaume Kukohoa Wanapopita Wanawake Wenye Maumbo Makubwa

Wasanii wa kike wamepta abahati ya kuongelea swala la polisi kutamka kuwa kutakuwa na ufatiliaji wa kisheria kuhusu tabia ya wanaume kuwa wanakohoa wanapoona wanawake wenye maumbo makubwa wanapopita .

Akiongea na waandishi wa habari, Snura anasema kuwa kwake yeye anaona ni swala la kawaida kwa sababu ameshazoea kufanyiwa hivyo lakini pia kama wameamua kukomesha tabia hiyo inabidi kuwa wanatumia maamuzi ya busara sana ili kufikia uamuzi wa kutoa adhabu.

Loading...

Sio baya lakini naona kama litakuwa gumu kidogo kutokanana kwamba mtuanweza kuwa anaguna kitu kingine na wewe ndo unapita,lakini katika kufanya maamuzi basi wafanye kwa kuangalia kabisa kuwa mtu huyo amefanya kwa makusudi yale wanayomaanisha wao, lakini kama kweli basi sawa lakini mimi nishazoea.

Alipoulizwa Shamsa Ford kuhusu maamuzi hayo ya serikali alisema kwake ni sawa tu kwa sababu kuna watu wamekuwa wakikosa uhuru na maumbile yao waliopewa na mungu kutokana na tabia ya vaadhi ya wanaume kuwa wanawazomea.

mimi haijawahi kunitokea na labda kwa sababu najua nivae nini   na wakati gani na wapi,lakini pia kama wameamua kufanya hivyo mi naona sawa tu  maana kuna watu hata wakivaa baibui mungu ndo wakajalia hivyo alafu akipita sehemu ndo anafanyiwa hivyo hiyo inawafanya wawe weak,washindwe kwenda baadhi ya sehemu kwa sababu ya maumbiel yake.mimi nimependa na wakazie mkazo hilo.-Alisema Shamsa Ford

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…