Mapambo Ufanya Nyumba Kuwa Nyumbani

Sio kila mmoja anaweza kuwa na nyumba yake na akaweza kukaa na kutulia nyumbani kwake muda wote, na pia wapo ambao upenda kukaa nyumbani muda wote na hata akafanya vitu vingi vya maana akiwa nyumbani bila kuwaza kwenda sehemu kufanya jambo hilo.

Haijalishi hata kama nyumba ni ya kupanga au unakaa kwenye chumba kimoja, upambaji wa sehemu unayokaa unaweza kukufanya kujivunia kuwa mahala ulipo .

download latest music    

angalia mtu anaweza kuna na nyumba kubwa lakini akapata kashughuli kadogo tu akawaza kukodisha ukumbi, kwanini usipange nyumba yako sawia na ukavutia watu wanaokuja kukuangalia au kufanya jambo fulani kwako.

Basi ukizingatia haya unaweza kupafanya nyumbani kwako kuwa  sehemu nzuri na hata kwa wageni wako pia.

Weka sanaa unayopenda.

Ushauriwa kuweka  nyumbani kwake kile kitu unachopenda, inaweza kuwa picha kubwa na nzuri ukutani inayoonesha jambo fulani kwako la muhimu la kumbukumbu au mtu wako wa karibu, au unaweza kutafuta kinyago au picha ya kuchora yenye rangi unayopedna na inayoendana na kuta za rangi yako.

jaribu kuweka mimea.

usishangae mtu anaweza kupanda  ua fulani sebleni kwako unakawaza kwanini kapanda mmea ndani, hapana siku hizi fashion imebadilika.kwa bahati nzuri Tanzania aina uhaba wa mimea , ipo ile inayokuwa taratibu na inayoweza kutunzwa kwa ufasaha inapokuwa ndani, jaribu kutunza mimea ndani ya nyumba yako .

vyombo vinavyoendana.

sio mbaya kuwa na seti zaidi ya moja ya vyombo nyumbani kwako ilimradi tu iwe na umaridadi na zinaendana kwa ukaribu zaidi, chagua rangi zote na zenye saizi zote,  hii itakufanya kuwa jasiri hata unapopata wageni nyumbani kwako.

kochi inayoleta faraja.

usisumbuke kununua thamani nyingi kwa wakati mmoja kwa sababu unadhani ni mtindo wa kisasa, jaribu kuwa na kochi nzuri sebleni hata kama ni moja au mawili lakini yenye rangi za kuvutia na zinazoendana na  rangi za ukuta na mapambo mengine pia.

kochi liwe lenye kukufanya upumzike unapokuwa unafanya mambo kadha wa kadha kama kuangalia TV,kusoma vitabu au kukaa na wageni muda mwingine.

Nyumba iwe na mwanga wa kutosha muda wote.

sio lazima iwe nyumba kubwa , hapana, hata sehemu ndogo kama utapangilia vizuri nyumba yako na kuweka mapambo mazuri na kuweza kuwa na mwanga wa kutosha basi ni nzuri zaidi, kuwe na hewa maridadi ya kukufanya upumzike na wala usiangaike wakati wote.

kumbuka kuwa nyumbani kwako kunaweza kuwa tofauti na kwingine kokote na ukapafanya sehemu muhimu kuliko zote za wewe kukaa na kupumzika kama tu utaweza kupaweka kama unavyotaka.kumbuka kuwa nyumba yoyote inaweza kuwa nyumbani kwa kubadilisha muonekano wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.