Mapya Yazuka Kuhusu Rav 4 Ya Hamisa

Mwanadada mrembo ambae amekuwa akionekana katika video za wasanii wakubwa mbalimbali nchini Hamisa Mobeto,bado anaendelea kutikisa vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali kutokana na scandal zake  na baba mzazi wa mtoto wake wa kiume, Hamisa ambae hivi karibuni alikuwa na scandal ya kusambaza picha za faragha za yeye na Diamond Platinumz ikiwa ni kama njia ya kuonyesha uthibitisho wa kile kilichokuwa kinasema kwa muda mrefu kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi.Hata hivyo baada ya picha hizo kuvuja msanii Diamond alikiri kuwa ni  kweli amezaa na Hamisa na kusema kuwa alinunulia hamisa gari aina ya Rav 4 .

Hivi karibuni zimeibuka tetesi mpya tena kuhusu gari hiyo aina ya Rav 4 na kusemekana kuwa gari hilo halikuwa zawadi kwa Hamisa Mobeto lakini lilikuwa limenunuliwa kwa ajili ya mama mzazi wa Diamond , baada ya kutokea Hamisa kujifungua ndipo ilipobidi kupewa yeye.Hata hivyo habari hizi bado hazijathibitika  na upande wowote wa wahusika, tetesi hizo zinasema kuwa gari hilo tangu lilipoagizwa lilikuwa na lengo la kupewa mama yake lakini kwa sababu lilifika kipindi ambacho ndio Hamisa anakwenda kujifungua ikabidi akabithiwe mrembo huyo.

download latest music    

Hata baada ya hamisa kutafuta ilishindikana kupatikana lakini mama mzazi wa mrembo huyoo , mama mobeto alipoulizwa kuhusu tetesi hizo alisema kuwa wameshazushiwa mambo mengi sana kwa sasa anaomba hasiliongelee hilo .

Hamisa Mobeto amekuwa kimya kwa muda tangu msanii Diamond kutamkaa katika vyombo vya habari kuhusu mahusiano yao, hata hivyo msanii huyo alikiri kumnunulia gari ilo mrembo huyo na kusema kuwa pamoja na kwamba alikuwa akimkana mtoto katika mitandao na kwa vyombo vya habari,bado alikuwa akiudumia mimba ya Hamisa vizuri kwa kumpa zaidi ya elfu 70 kwa wiki, na hata kabla ya kujifungua alimpa millioni 7, na alipojifungua alimpa laki tano. Wawili hao kwasasa inasemekana kuwa hawapo katika mahusiano mazuri pamoja na kwamba wameshaunganishawa na mtoto, Hamisa alitaka kulipwa milioni mbili na laki tano kila wiki ikiwa kama matunzo ya mtoto , lakini baada ya Diamond kwenda kwa wanasheria kwa sasa anatoka laki mbili kama matunzo ya mtoto.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.