“Marafiki Wabaya Walitaka Kumpoteza Wema”-Mama Wema

Mama mzazi wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Bi. Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amefunguka na kuwataja marafiki kama watu waliokuwa wanampoteza Wema.

download latest music    

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mama Wema Mama Wema alimuongelea binti yake Wema  ambaye kwa sasa amekuwa kimya huku akionekana kufanya mambo ya maendeleo ikiwemo kufungua duka lake la nguo lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

Wale watu waliomzunguka hawakuwa sahihi, alikuwa na msururu wa watu wakufuata tu mkumbo, wanafuata tu kama mkia vile.

Wema anapendwa, hata hawa unaowaona kila siku wanampinga kwenye mitandao ya kijamii sio kwamba wanampinga, wanampenda sema Wema anakuwa hajui tu“

Lakini pia Mama Wema alifunguka mapenzi aliyonayo kwa binti yake na kumpongeza kwa kufungua duka lake jipya:

Walimpinga hata katika suala hili la duka lakini namshuru Mungu amefanikiwa, amelifungua tayari na leo (juzi) amenialika niende kuona.

Mimi huyu ni mwanangu, nampenda sana na ndio maana hata afanye nini bado nitaendelea kuwa naye bega kwa bega, naamini kabisa sasa hivi ameachana na marafiki wasiofaa na amebadilika”.

Wema amekuwa kimya sana tangu skendo yake ya kusambaza picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii ambapo kesi yake bado inaendelea kusikilizwa mahakamani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.