Mashabiki Wamtolea Povu Lulu kwa Kutomzika Patrick

Ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu maziko ya mtoto Patrick yamepita ambapo maiti ya mtoto huyo iliagwa katika uwanja wa Leaders na kuacha simanzi kwa watu wengi sana. Maombeloezo hayo yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali huku wimbi kubwa likiwa ni wasanii walifurika katika viwanja hivyo.

Lakini kesi imekuja baada ya mashabiki kuanza kuhoji kwamba kwanini mtu muhimu na wa karibu na Muna Love , Lulu Michael hakuhudhuria katika kuagwa  kwa mwili huo katika viwanja hivyo ilhgali kuna video zilivuja zikimuonyesha lulu akiwa nyumbani kwa muna akiwa anaandaa sehemu kwa ajili ya wageni wanaokuja katika msiba.

download latest music    

Wengine wamesiitishwa hasa wanaojua maisha ya nyuma ya lulu na uhusiano aliokuwa nao na baba mzazi wa marehemu( Peter) ambae aliangaika sana na Muna kipindi cha kesi yake ya mauaji iliyokuwa imemsumbua sana msanii huyo.

Watu waliokuwa msibani , baada ya kuona video ile walitegemea kuwa lulu atakuwa karibu sana na Muna kutokana na pia Muna alivyokuwa akijitoa sana katika matatizo ya Lulu hata kipindi mtoto wake akiwa mgonjwa hospital.

Baadhi ya watu waliokuja msiba waliongea sana kuhusu hilo huku wengine wakisema kuwa kwa sasa  lulu hakuwa amepanga kutokea hadharani kwa watu na ndio sababu inamuwia vigumu kutokea kwa ghafla ukizingatia hajamaliza kifungo chake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.