Master J Adai Ma-Prodyuza Hawalipwi Vizuri Kama Zamani

Producer mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Joseph Kimario maarufu kama Master J amefunguka na kuweka wazi kuwa watayarishaji wa muziki wa sasa hawalipwi vizuri kama ilivyokuwa kwao siku za nyuma.

Master J alijizolea umaarufu kutokana na kutengeneza hits songs kibao kwa wasanii wakongwe Kupitia Music Label yake ya MJ Records.

download latest music    

Kwenye mahojiano yake na EFM, Master J amefunguka na kusema kwamba kuna watayarishaji wengi wahalipwi vizuri kuliko wale ambao wanalipwa vizuri kidogo.

Maproducer wengi hawapati kitu, yaani msanii akikuheshimu sana atakupa laki mbili au laki tatu lakini hawa wengine wote ni laki kushuka chini wimbo mzima mpaka beat”.

Lakini pia Master J amewataka Maprodyuza kuhakikisha wanakuwa wabunifu ili kutengeneza Muziki utakaosanifu uhalisia wa Bongo fleva:

Kiukweli Muziki wetu umepoteza uhalisia tunakopy sana kutoka kule Nigeria, Maproducer waongeze ubunifu kidogo ili tuweze kuwa na aina ya Muziki wetu . Kwa maana hili sio zuri maana tuna makabila Zaidi ya 120 tunaweza kuchanganya na kupata uhasilia wetu” .

Master J alitangaza kuachana na kutengeneza muziki na kuamua kuangalia biashara zake nyingine  na kuwakabidhi MJ Records vijana wengine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.