Loading...

Matonya aeleza sababu ya kuhamia Kenya

July 17, 2017 at 15:07
Matonya aeleza sababu ya kuhamia Kenya

Matonya amepinga uvumi kuwa alitoroka Tanzania kwenda Kenya kwasababu anatakikana na polisi kuhusu kesi ya utumizi wa dawa za kulevya.

Hit maker huyo ambaye anajulikana kwa nyimbo kali kama ‘Vaileti’ na ‘Anita’ alidhibitisha kuwa amehamia Kenya akizungumza na vyombo vya habari nchini humu.

Matonya alieleza kuwa yeye hajatoroka mkono mrefu wa serekali kwani yeye hatumii dawa za kulevya na wanaodai hivyo wanamchafulia jina tu.

“Sijatoroka Tanzania kwasababu hiyo, unaona hata listi ambayo imetajwa Matonya hakuwa pale. Matonya ni mtu safi na hizo ni stori zinakuwa kwa ajili ya kuniharibia jina,” Matonya alisema.

Matonya alieleza kuwa alihamia Kenya kwasababu anajihusisha na biashara kadhaa ikiwemo biashara ya kununua na kuuza gari.

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere