Maua Sama Afungukia Mafanikio Ya ‘Iokote’

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Maua Saleh maarufu kama Maua Sama amefunguka na kuongelea mafanikio ya wimbo wake wa ‘Iokote’ ambao unaendelea kufanya vyema.

Licha ya Maua kufanya nyimbo kadhaa nzuri huko nyuma lakini wimbo wake wa ‘Iokote’ ndio umekuwa kama umemtambulisha sana Kwenye ulimwengu wa Bongo fleva.

download latest music    

Katika mahojiano yake na Global Publishers , Maua aliyeimba wimbo huo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu Banza Stone, Hanstone alisema kuwa, katika maisha yake hajawahi kutegemea kama ataachia wimbo wa kumchanganya kiasi hicho ambapo tangu autoe umezidi kumpa shoo hadi anachanganyikiwa.

Yaani sijui hata nisemaje, Iokote imenifanyia maajabu makubwa sana hata nashindwa nielezeaje, kama huko nje ya nchi hadi sasa napata shoo hadi nachanganyikiwa nitajigawaje. Ukiingia mitaani, kwenye usafiri ndiyo nakuwa chizi kabisa”.

Licha ya mafanikio aliyopata Maua Sama Kupitia wimbo huo Lakini pia alipitia kipindi kigumu mara baada ya kuwekwa rumande kwa muda wa wiki nzima baada ya kukamatwa

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.