Maua Sama Akana Kutumia Uchawi Kupata Mafanikio

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kutumia nguvu za giza ili kupata mafanikio katika kazi zake za kimuziki.

Maua ametoa siri ya mafanikio yake na kusema ni Mungu pekee ndiye amempa mafaniko katika kazi zake za kimuziki.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Maua alisema anachoamini siku zote kwenye maisha yake kuwa wakati wa Mungu ndio sahihi siku zote hivyo mpaka wimbo wake huo unatokea kupendwa hivyo ni kwamba amewapa mashabiki wake wanachotaka.

Unajua mtu mwingine anaweza kujua ni uchawi kumbe sio kabisa ni muda sasa wa Mungu ameamua kukurudisha kwa kasi kwa mashabiki wako na hicho ndio kitu muhimu sana”.

Maua amezidi kung’aa na wimbo wake huo ambao umekuwa ukihit sana na mpaka sasa unashukilia chati katika vituo mbali mbali vya redio an televisheni lakini pia kuwa na watazamaji mamilioni katika mtandao wa Youtube.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.