Mbosso Afungukia Bifu Lake na Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema chini ya Label ya WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa hali sio shwari kati yake na msanii mwenzake Aslay.

Mbosso ameweka wazi kwamba kwa sasa hayupo sawa na muimbaji mwenzake, Aslay ambaye awali alikuwa anafanya naye kazi katika bendi ya Yamoto Band.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Azam, alisema kuwa awali alikuwa anamsupport Aslay katika kazi zake ambazo amekuwa akizitoa lakini yeye amedai alikuwa hasapotiwi na muimbaji huyo.

Baada ya kumsupport Aslay kwa muda mrefu watu wakawa wananimbia mbona wewe unam-support halafu yeye haku-support? umem-follow mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalance shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea ngoja na mimi nim-unfollow. Kwa hiyo sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake”.

Aslay na Mbosso walikuwa katika Kundi moja la Yamoto Band kwa miaka mingi Lakini walikuja kutengana  kutokana na sababu za kimaslahi ambapo Mbosso alijiunga na Label ya WCB.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.