Loading...

Mbosso Afungukia Ukaribu Wake na Esma Platnumz

October 02, 2018 at 07:14
Mbosso Afungukia Ukaribu Wake na Esma Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Label ya WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuelezea uhusiano wake na Dada wa CEO wa WCB Diamond Platnumz, Esma Platnumz.

Mbosso na Esma wameonekana kuwa na ukaribu sana hasa Kwenye mitandao ya Jamii ambapo wamekuwa waki piga picha mara kwa mara na kuzirusha mtandaoni.

Loading...

Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari, Mbosso amesema Esma ni mshikaji wake sana na huwa wanaimba wote baadhi nyimbo na mara nyingi humfundisha kuimba pia hufikia kipindi hadi anamshawishi na yeye aweze kuimba yaani ajiingize kwenye mambo ya muziki.

Lakini pia mbali na kuongelea ukaribu wake na Esma lakini pia amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zinasema kuwa yeye ana mahusiano na dada mwingine wa Diamond ambaye pia ni msanii Queen darlin,na kusema hama mahusiano nae kabisa.

 

Share

Comments

  1. Esma ni mzee bana

  2. Man from Mars : October 2, 2018 at 9:32 am

    Wewe mbosso hebu waheshimu wazee wako

  3. Yetu macho tu

  4. Aisee hawa wamama hawalali yaani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…