Mc pilipili Amewadhalilisha Wanaume Wote :-Mwijaku

msanii wa maigizo maarufu kama mwijaku amefunguka na kumtupia lawama msanii mwenzake upande wa vichekesho mc pilipili kwa kitendo alichokifanya wikiend hii na kumuita kuwa ni zuzu.

Mc pilipili ambae aliweza kumvalisha pete mchumba wake phinomena wikiendi iliyopita na kuzua gumzo sana kutoka katika mitandao ya kijamii kwa sababu alimwaga machozi kipindi akimvalisha pete mwanamke huyo kitu ambacho hakikuwa cha kawaida katika matendo hayo.

download latest music    

Mwijaku anasema kuwa alichokifanya MC pilipili ni kuwa zuzu kwa sababu huwezi kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke na kwmaba amewadhalilisha wanaume wote wa dar kutokana na kitendo icho.

Mwijaku anasema kuwa kulia sio dhambi lakini dhambi ni pale unapolia mbele ya watu lkwa sababu ya mwanamke.

Sio dhambi kulia, dhambi ni kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke .

Hata hivyo Mwijaku anasema kuwa amekuwa akimfahamu sana Mc pilipili naamekuwa akimueleza mengi kuhusu yake anayoyapitia katika mahusiano yake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.