Mc Pilipili Ampigia Magoti Rose Ndauka

Mc Pilipili ampigia magoti Rose Ndauka kumuomba radhi hadharani baada ya actress huyo maarufu kuwa mkali kwa kumburuza kwa wanasheria kumtaka amlipe million 150 za Kitanzania kwa kumchafua mbele ya umma kuwa ameshatembea nae kimapenzi huku akijua sio kweli anadanganya jamii

Katika barua iliyoandikwa tarehe 9 January 2019 na wanasheria kutoka kampuni ya KIKA Attorneys ya jijini Dar es salaam inamtaka Mc Pilipili kumuomba radhi Muigizaji huyo kwenye media hizo hizo alizotumia kumchafua mteja wao ambapo Rose anakiri taswira yake mbele ya jamii kuchafuka kwa matamshi ya Pilipili. Asipoomba radhi hatua zaidi zitachukuliwa kulipa fidia ya million 150 kumchafua muigizaji huyo

download latest music    

Barua hiyo ya wanasheria wanaomuwakilisha Rose inasema asilimia 70% ya kazi zake za Sanaa na biashara nyingine anazofanya hutegemea reputation ya Jina lake alilojijengea kwa miaka takribani kumi sasa hivyo ameanza kuathirika ikiwemo kukosa deals kadhaa kwa kuchafuliwa huko. .

iSku chache zilizopita baadhi ya watu walikuwa wakimdhihaki na kumkejeli mitandaoni Rose kufuatia mc Pilipili kumchumbia mwanamke mmoja wakidhani rose ni zilipendwa wa mc Pilipili kumbe si kweli. Juzi Kwa Mara ya pili Rose aliandika kumtaka Mc Pilipili aseme ukweli asiendelee kuchafuka lakini hakufanya hivyo kitu ambacho kinaashiria Rose kwa Mara ya Tatu kuamua kufuatia proffesional route zaidi kwa wanasheria badala ya kumbembeleza Mc Pilipili

Katika nyakati tofauti kuanzia 2016 MC Pilipili kwenye interviews na media mbalimbali alikuwa akijitapa kutembea kimapenzi na baadhi ya wasanii maarufu wa kike akiwemo Rose Ndauka ambapo mwaka 2016 Rose alikanusha kutembea na Pilipili lakini mchekeshaji huyo aliendelea kusema ametembea na actress huyo aliyejipatia umaarufu sababu ya kazi zake za Sanaa

Leo MC Pilipili amepost kumuomba radhi Rose lakini akiwa amezuia comments section watu wasitoe maoni Yao

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.