Mchekeshaji Ebitoke afunguka kuhusu Ben Pol kushindwa kumuondoa ubikira

Mchekeshaji wa kike Ebitoke alipata umaarufu sana miezi michache zilizopita alipolia kwenye mahojiano kwa TV huku akitaka msanii Ben Pol afunge naye ndoa.

Ebitoke alisema anampenda sana Ben Pol na hata alitaka mwimbaji huyo amuondolee ubikira wake. Alisema alikua tayari kufanya lolote ili Ben Pol ampende.

download latest music    

Soma pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ben Pol na Ebitoke hatimaye walikutana na kwa sasa inasemekana kuwa wawili hao ni wapenzi. Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) ya EATV, Ebitoke alisema kuwa Ben Pol hajafanikiwa ‘kufungua mlango wake’.

Ben Pol na Ebitoke

Mchekeshaji huyo alieleza kuwa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake na alitaka Ben Pol ndo awe mwanaume wa kwanza kulala naye.

Hata hivyo kuna wale wanaodai kuwa Ben Pol na Ebitoke wanafanya tu utani ilhali wanazidi tu kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere