Mchekeshaji Mc Pilipili apata ajali ya gari

Mchekeshaji maarufu nchi  Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili jana tarehe 12 septemba alipata ajali ya gari katika barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza.Mchekeshaji huyo ambae kwenye gari w alikuwa na watu wengine wawili na yeye  watatu huku dereva akijulikana kwa jina la Said Hassan. Ilielezwa kuwa gari aina   ya Prado ndio lililohusika kwenye  ajali iyo maeneo ya Bubiki mkoani Shinyanga na watu wote walikimbizwa haraka sana katika Hospitali  ya Rufaa ya  Bugando iliyopo mkoani Mwanza.

Hata hivyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Shinyanga  kamanda wa polisi mkoani humo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema kuwa chanzo cha ajali aliyoipata  Mc Pilipili na wenzie  ni kuwa alikuwa anamkwepa mtoto mdogo aliyekuwa akiendesha baiskeli lakini pia dereva ya gari hiyo alikuwa katika mwendokasi,katika kuelezea ajali iyo  kama huyo anasema kuwa gari iliacha njia na kupinduka .mc pilipili amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwa ni pamoja na sehemu za kifua.Kwa upande wa dereva aliumia sehemu za mkononi ,mkono wa kulia  na majeraha wote wapo hospitali hapo kwa matitababu zaidi .

download latest music    

Akiongea na mwandishi wa gazeti la mwananchi,Ofisa Uhusiano wa  hospitali hiyo ili kuelezea hali yake  alisema kuwa   ni kweli wamempokea katika kitengo cha dharura na amehudumiwa, hali yake bado haijaimarika na kwa sasa Mc Pilipili yupo chumba cha wagonjwa wanaitaji uangalizi zaidi huku wakiendelea kumfanyia vipimo vingine.

Inaelezwa kuwa mc pilipili alipata ajali iyo alipokuwa anatoka Shinyanga kwenda Mwanza ambapo alikuwa amearikwa katika kusherekea harusi mkoani humu,

Kwa kudhiirisha taarifa hizo wasanii na watu mbalimbali katika tasnia yake wamekuwa wakiposti picha katika kurasa zao za instagram  za mchekeshaji huyo maarufu huku wakimtakia apone haraka na wengine wakimpa pole kwa kupata ajali, lakini pia  baadhi yao pia wameonekana wakitoka hospitali kumjulia hali ikiwepo Belle 9, na  Katarina Karatu ambao walipata bahati ya kwenda kumjulia hali.Tunamtaki Mc Pilipili afya njema na apone haraka.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.