Mchepuko Adaiwa Kuwa Tishio Kwenye Ndoa Ya Dogo Janja na Uwoya

Ndoa ya staa wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Banana’ na Bongo Movie Star Irene Uwoya yadaiwa kupumulia mashine huku mchepuko akiwa chanzo.

Global Publishers wanaripoti kuwa ndoa Changa ya mastaa hao imedaiwa kuingia jini mkata kamba baada ya Mrembo anayeitwa Dayana kudaiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Dogo Janja.

download latest music    

Chanzo cha karibu cha couple hiyo kiliitonya GPL kuhusiana na tatizo katika Ndoa hiyo ya Dogo Janja na Uwoya:

Fuatilieni, Uwoya na Dogo Janja hawako sawa kabisa chanzo ni Dayana, nasikia wanawasiliana sana na mara kadhaa Dogo Janja ameshindwa kuvumilia hadi kumposti kimafumbo kwenye ukurasa wake wa Instagram”.

Baada ya Tetesi hizo Dayana alidaiwa ili kujibu tuhuma hizo lakini hakutaka kukubali wala kukataa lakini alimpa ujumbe mzito Uwoya:

Ningepanda sana kumshauri dada yangu Uwoya kuwa kwanza amsihi mumewe asiwe ananisumbua kwa simu kwa sababu mimi niko na mtu mwingine lakini najua atapata naye tabu sana kwa sababu Dogo Janja bado mdogo hivyo bado hajafika kwenye safari ya mapenzi.

Nafikiri ingekuwa vizuri kabisa Uwoya angemtafuta mtu ambaye analingana naye lakini hivi sio sawa atapata tabu sana ni bora kuwa na mtu mzima mwenzake”.

Baada ya GPL kuzungumza na Dayana, lilimtafuta Uwoya ili kusikia anamzungumziaje ‘mwizi’ wake ambaye pia amempa ushauri ambapo alipopatikana hakutaka kufunguka kwa kirefu zaidi ya kusema amepokea ushauri wake.

Sidhani kama kuna kitu kikubwa cha kusema ila tu nashukuru ushauri wake nimeupokea nitaufanyia kazi“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.