Mchungaji Aliyefufua Mtu Afrika Ya Kusini Kushitakiwa

Mchungaji mchungaji wa Afrika Kusini Alph Lukau ambaye inasemekana alimfufua mtu siku ya jumapili ya february 21 ameibua gumzo dunia nzima.

Hivi sasa inasemekana kuwa kampuni ya uuzaji wa masunduku ya mazishi nchini humo imejitokeza na kusema wanafikiria kumshtaki mchungaji huyo.

download latest music    

Mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha Kings and Queens, kinachojihusisha na mazishi, Bi.Vivian Mponda amefanya mahojiano na kituo cha habari cha SABC nchini Afrika kusini, ambapo amesema wao walifuatwa na mmoja wa wanafamilia wakiomba kutumia usafiri, lakini sanduku lililotumika halikuwa la kwao na wala mwili huo haukuhifadhiwa hapo kama wanavyodai, kwani huwa hawahifadhi mwili bila taarifa rasmi.

Hatukuwauzia sanduku hivyo sio la kutoka Kings & Queens na hatuna sanduku la vile kwenye mochwari yetu, ila gari walikodi kwetu wakisema wanataka kulitumia kwenye mazishi ya ndugu yao”.amesema Ms. Vivian.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji (SABC) habari zinasema kwamba waandishi walimfuatilia mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Eliot na mpenzi wake ambaye alikuwepo siku ya tukio (kufufuliwa), na kugundua kuwa waliondoka nyumbani kwao tangu Jumatano, na hawajarudi mpaka sasa.

Wakiendelea kuchunguza hilo imebainika kuwa hata mtu aliyesema amempangisha nyumba yake ambaye ndiye alimfia mikononi sio kweli, kwani mwenye yeye ni mwanamke na aliyekuwepo siku ya tukio hilo alikuwa ni mwanaume.

Jumapili ya Februari 24 mchumgaji Alph Lukau wa kanisa la Aleluia Ministry la Afrika Kusini amezua mtafaruku mkubwa mitandaoni baada kudai amemfufua mtu, aliyeletwa na mwenye nyumba wake akidai kuwa alifariki baada ya kumkimbiza hospitali alipoumwa, na ndipo akaamua kumpeleka kanisani kumuombea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.