Mdau wa Elimu Kumsomesha Mtoto wa Agness, Wasanii pia Wachangia Elimu Yake

Mdau mmoja wa elimu mkoani Mbeya amejitokeza na kujitolea kumsomesha mtoto wa marehemu agness masogange mpaka chuo kikuu kuanzia mama yake alipoishia.Akiongea siku yajana katika mazishi ya msiba wa agness masogange mdau huyo wa elimu aliguswa sana na msiba wa mrembo huyo lakini pia aliguswa sana na harakati zake za kimaisha alizokuwa amepitia Agness mapka kuwa maarufu.

download latest music    

SANIA, MTOTO WA MAREHEMU AGNESS

Ukiachana na mdau huyo wa elimu kuamua kumsomesha mtoto huyo lakini pia, wakati akitoa risala ya mwsiho a marehemu katika viwanja vya Leadrs Club, Zamaradi alisema kuwa mtoto wa Agness yuko darasa la saba kwa sasa na kama bongo movie waliamua kuchanga milion  2 ambazo zitaweza kumsaidia katika masomo yake kwa kipindi kifupi.

Lakini pia akiongea na waandishi wa habari, Rammy Galis ambae aliwahi kuwa mpenzi wa Agness Masogange anasema kuwa  watanzania wanapaswa kujua kuwa mtoto wa Agness ni wa kwao wote hivyo kwa yoyote aneguswa na msiba huo basi inabidi kumsaidia kwa sasa kwa sababu mama yake ndio alikuwa nguzo kubwa maishani mwake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.