Mdogo wa Kanumba Atoa Ushahidi Kesi Ya Lulu

Ikiwa ni kama muendelezo wa kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya mfalme wa bongo moves Steven Kanumba, kesi inayomkabili aliyekuwa mpenzi wake ambae pia kwa sasa ni malkia wa bongo movies na amekuwa akifanya vizuri sana katika kazi yake Elizabeth Lulu Michael, shaidi wa kwanza ametoa ushahidi wake oktoba 19 kuhusu alichokuwa anakijua kuhusu mauaji hayo.

Seth Bosco ambae ni ndugu wa marehemu kanumba alitoa ushahidi wa kile kilichotokea katika kifo hicho miaka mitando iliyopita, akitoa ushahidi huo mbele ya mahakama, Seth Bosco alisema kuwa siku ya tukio la kifo cha Kanumba wawili hao walikuwa na mgogoro ambao ulisababishwa na msanii Lulu Michael kuongea na simu na na simu hiyo ilisadikika kuwa ni ya mwanaume mwingine.

download latest music    

Mbali na Seth Bosco, kulikuwa na shahidi mwingine ambae ni daktari aliepokea mwili wa marehemu ambae siku ya jana hakuweza kufika kutokana na hudhuru ya kuumwa, hata hivyo shahidi huyo anatarajiwa kufika mahakamani kwa ajili ya ushahidi siku inayofuta ya tarehe 20.

Baadhi ya watu walihudhuria mahakamani hapo ni pamoja na Muna akiwa kama rafiki wa karibu wa familia ya Lulu Michael,Dk.Cheni, mama mzazi wa Elizabeth Lulu Michael ,a mama mzazzi wa Kanumba ambae muda wote alionekana kuwa ni mtu  hasiye na furaha.

Steven Kanumba na Elizabeth Michael walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ,Kanumba alifariki April 2012 baada ya kuanguka kulikosadikika kulisababishwa na ugomvi  aliokuwa nao na mpenzi wake huyo.Hata hivyo ksi hiyo inayomkabili Lulu Michael ni kesi ya kuua bila kukusudia.Kesi ya Lulu itaendelea leo tarehe 20 Oktoba 2017.

Mungu awatie moyo familia zote zinazohusika katika kesi hii.

Elizabeth Michael  akiwa mahakamani

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.