Mfahamu Vizuri Madame Wema Isaac Sepetu

Wema Abraham Sepetu,alizaliwa tareh 28 Septemba mwaka  1988,  Wema ni mwanamitindo, muigizaji na pia  ni mjasiriamali, mwaka 2006 Wema alishinda taji la Miss Tanzania.

Wema ni mtoto wa nne na wa mwisho katika familia ya mzee Abraham Sepetu, elimu yake yote Wema Sepetu amesoma katika shule ya  ‘Academy International’ iliyopo jijini Dar Es Salaam, na baadae kwenda Malaysia alipoenda kusomea uongozi wa biashara.

download latest music    

Ukiachana na elimu yake na ushindi alioupata katika ulimwende , Wema ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania , ni mmoja wa wasanii wakubwa na wakongwe ambao bado wanaendelea kufanya vizuri katika tasnia, moja wa watu wa karibu waliogundua kipaji cha Wema  ni marehemu Steven Kanumba, huku akionekana kucheza nae vizuri katika baadhi ya movie ikiwepo ‘The Point of no Return’.Na hivi karibuni  alizindua movie mpya ya ‘Heaven Sent’

Wema amekuwa moja ya wasanii wa kike wenye ushawishi mkubwa sana wa watu hasa katika mtandao, ni mwanadada mwenye moyo wa kupendwa na watu lakini ameonekana kuwa siku zote ni mvumilivu pamoja na matatizo mengi anayokumbana nayo.Mara nyingi amekuwa akisema vibaya lakini haonyeshi kujali kwa maneno ambayo watu wamekuwa wakimsema.

Msanii huyo bado hajabahatika kuolewa lakini ameshapitia katika mahusiano na baadhi ya wasanii maarufu kama Mr.Blue, Diamond Platinumz, Charls Baba, T.I.D, na wengi maarufu lakini kwa sasa mahusiano yake hayawekwa wazi sana ingawa kuna tetesi za kuwa na mpenzi mpya ambae sio maarufu.

Akiwa kama msanii na kipenzi cha watu wengi, inaweza  kusemekana kuwa Wema ndio msanii wa kwanza Tanzania kuwa na kundi la watu wanaompenda katika mtandao linalojulikana kama “team wema”, ambao wamekuwa wakimsapoti karibia katika kila anachokifanya lakini pia ndio watetezi wake wakubwa mara mashabiki wasiompenda wanapomuandama.

Katika upande wa uajsiriamali, wema alikuja na bidhaa yake ya lipstick iliyojulikana kama “Kiss by Wema Sepetu”, ambayo iliopoingia sokoni ilipendwa sana na wanunuzi, Wema pia alikuwa na kipindi cha Tv show ambacho kwa sasa kimesimama kidogo.

Inawezekana ikawa ni hitaji lake lakini sio muhimu sana kwa sasa, kwa muda Wema amekuwa akiandika katika mitandao juu ya kuomba Mungu ili apate mtoto, ambapo wanawake wengi kwa umri kama wake wamekuwa na watoto sasa,ikiwa leo ni siku anayoadhimisha siku ya kuzaliwa kwake basi tunamuomba Mungu amtimizie haja ya moja wake na mafaniko kwake.HAPPYBIRTHDAY WEMA!!!

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.