Mh Makonda Aanza Kusaidia Matibabu ya Pascal Cassian

Aliyewahi kuwa mshiriki na mshindi wa shindano la BSS Pascal Cassian amekuwa hoi kitandani kwa muda mrefu huku akiomba msaada kwa watu na wasanii wenzake lakini swala hilo lilishindwa kufanikiwa, hata hivyo mke wake amekuwa akipiga kelele sana katika vyomba vya habari kutaka kuomba msaada kwa watu ili aweze kutibiwa.

Hata hivyo kwa muda mrefu sasa tangu ameanza kuomba msaada na hakuna aliyekuwa tayari kufanya hivyo lakini mkuu wa mkoa, Mh Paul Makonda ameamua kujitoa kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo ambapo ameanza kutibiwa.

download latest music    

Msanii huyo siku ya February 19 alianza kwa kuapatiwa matibabu katika hospitali ya muhimbili na kisha kuamishiwa katika hospitali ya mloganzila kwa ajili ya vipimo zaidi.

Lakini bado msanii huyo anahitaji msaada sana kutoa kwa watu na wadau mbalimbali.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.