Mimi Mars Afunguka Tetesi za Vee Kuwa Mjamzito.

Msanii wa muziki  bongo fleva mimi mars amefunguka na kumtetea dadake vannesa mdee kutokana na tetesi zilizokuwa zimezuka siku za nyuma kidogo kuhusu Vannesa kuonekana kuwa ni mjamzito,Mimi Mars amesema kuwa dada ake amekuwa akila sana kwa sasa hivi na ndio maana amekuwa akiongezeka kila siku lakini sio kwamba vee ana mimba.

Akiongea na Funiko base ya Radio Five, Mimi Mars anasema kuwa kupenda kula kwa Vannesa kunasababisha watu kuhisi kuwa dada ake ni mjamzito lakini sio kweli na ni kitu ambacho hakiwezekani.

download latest music    

Hapana haiwezi kutokea,namuoa kila siku ni kwamba  anakula sana, mahaba ni mengi sana kwaio wanafurahia sana lakini sio hivyo na wala hana mimba .-Alifunguka Mimi Mars.

Vannesa ambae yuko katika mahusiano na msanii mwenzake Jux wamekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu ambapo siku za nyumba ilitokea picha iliyomuonyesha Vannesa sehemu yake ya tumbo kuwa kubwa  na kusababisha watu kuhisi kuwa ni mjamzito.

Mimi Mars na Vannesa ni ndugu wa familia moja na wamekuwa karibu katika kusaidia kimuziki ingawa hawajawahi kufanya kazi ya muziki kwa pamoja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.