Mimi Mars: Sina Papara Na Mapenzi

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa na ngoma yake mpya ya papara Mimi Mars amekiri kuwa hana haraka ya kihivyo ya kuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.

Mimi Mars aliyejipatia umaarufu na ngoma yake ya kwanza ya shupa Lakini pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee, amekiri kuwa ana pressure kubwa ya kuwa kwenye mahusiano na kuyaweka public kutoka katika mashabiki zake.

download latest music    

Siku za hivi karibuni Mimi Mars alikumbwa na skendo ya kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz na hata rapa Joh Makini na hata shemeji yake Jux Tetesi za Mahusiano ambazo alizikana.

Kwenye Interview aliyofanya na Bongo 5 Mimi Mars amefunguka pia hata kama akiwa Kwenye Mahusiano hatapenda kuweka kila kitu public bali atataka Mahusiano Yake yawe private:

Hapana kwa sasa siko kwenye mahusiano lakini naona hata kama nikiingia Kwenye Mahusiano itakuwa ngumu kwangu mimi kuyaanika kwa sababu naona tayari maisha yangu yote yako public kwaiyo nitataka hata nikirudi nyumbani niwe na angalau kitu changu peke yangu ambacho mimi mwenyewe nakijua na pia inanisaidia maana ni kuweka mahusiano wazi inanisaidia kidogo maana Mahusiano hakuwa wazi inaleta matatizo kidogo”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.