“Mimi na Wema Tutaenda Kumtembelea Muna Labda Tufukuzwe”- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere ameweka wazi kuwa hana kinyongo na Muna hata baada ya povu alilomtolea Povu Kwa waandishi wa habari Lakini ameshapanga kwenda kumtembelea.

Sakata hili lilianza wiki chache Kwenye msiba wa mtoto wa Muna ambapo Steve alionekana kuingilia mambo ya kifamilia ya Muna na kutangaza Kwenye mitandao ya kijamii taarifa ambayo Muna amedai haikua ya kweli.

download latest music    

Lakini siku ya jana Steve ametangaza kumsamehe Muna na kudai anajua hiki ni kipindi kigumu kwa Muna kwani bado anamuomboleza mtoto wake hivyo haoni sababu ya kuweka kinyongo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve  amedai kuwa yote ambayo ameongea Muna siku ya jana kuhusu yeye sio ya kweli na tayari ameshamsaheme ambapo amepanga safari ya kwenda kumtembelea akiwa na Wema Sepetu.

https://www.instagram.com/p/BlaXDuthZLR/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1lebqzhdtqbzi

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.