Miss Bella Ashambuliwa Baada ya Kutangaza Mahusiano Yake na Godzilla

Mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii wamekwaza na uamuzi wa mwanadada Miss bella baada ya mwanadada huyo kuamua kusema ukweli kuwa alikuwa msichana wa mwisho wa mwanamuziki Godzilla ambae amefariki usiku wa kuamkia February 13.

Hisia za mashabiki zinakuja juu baada ya mwanadada huyo kuamua kuandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa amekuwa na mahusiano  na msanii huyo ilihali hapo awali kipindi akiwa hai hakuwahi kusema swala hilo na alikuwa akikanusha katika mitandao ya kijamii.

download latest music    

Bella ambae aliwahi kusikia akisema kuwa mahusiano yake na God ni kama kaka na dada alafu leo hii anasema ukweli inazidi kuwachafua mashabiki ambao kwa sasa wapo katika majonzi.

Hata hivyo , mwanadada bella anaonekana kuwa na taarifa tofauti na zile za familia kuhusu kifo cha msanii huyo hasa familia inaposema amefia nyumbani huku yeye akisema kuwa alifia hospitali Lugalo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.