Miss Shinyanga Aelezea Sababu Za Kumchukia Mc Pilipili

Msanii wa kike wa nyimbo za injili Nicole Franklin Sarakikya ambae pia alishawahi kushiriki mashindano na kushinda Miss Shinyanga  amefunguka na kuelezea kuhusu mahusiano yake na kukubali juu ya baba wa mtoto wake,Nicole ambae ana mtoto mmjoa wa kiume aliyezaa na mbunge wa singida Ery Kingu, anakubali kuwa ndie baba wa mtoto na anasema kuwa baba  huyo anamuhudumia vizuri mtoto wake  lakini kwa sasa hawana mahusiano ya kimapenzi ila wanawasiliana kama wazazi. ” ni kweli Erry Kingu ni baba wa mtoto wangu , Gideon” alisema Nicole

Kuhusu yeye kujua kuwa baba wa mtoto ni mume wa mtu nicole anasema kuwa ana muheshimu sana mke wa mzazi mwenzie “namuheshimu sana yule mama , she is so humble na sijui kama anajua”

download latest music    

Katika mahojiano yake na Spin Tv, anasema  sababu za yeye kuachana na baba mzazi wa mtoto wake al “hata sijui sababu,  mara nyingine hutokea, watu wanaachana bila kuwa na sababu labda yeye anajua, na wala sijutii kuwa nae kwa sababu amenipa baraka, mtoto ni baraka”

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Nicole alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchekeshaji na mshereheshaji maarufu Mc Pilipili , lakini alipoulizwa kuhusu Mc Pilipili, Nicole alikataa kumuongelea huku akisema kuwa hakuna  kitu chochote cha maana kitakachomfanya yeye amuonglee Mc Pilipili tofauti na Ery ambae wana bond ya kuwa na mtoto tayari katika maisha yao.

“Kitu kikubwa kilichonichosha kwa Mc Pilipili ni kujenga urafiki na baba wa mtoto wangu na kunisnitch” aliongea Nicole.Anaendelea kusema kuwa hata alipokuwa akiongea na Mc Pilipili kuhusu matatizo yake na Ery bado alikuwa anayafikisha kule kwa muhusika “thats was too  bad na icho  ndo kilichofanya nimemchukia”

Kwa Nicole , ni sawa kwa  baba wa mtoto  wake kuwa na urafiki na ex  wake lakini sio mpaka wafikie hatua ya kumuongelea yeye,hata kama ni kwa  faida zake lakini anakerwa na tabia ya ya Mc Pilipili kuingiza mambo yale katika urafiki wao.Nicole anasema kuwa kitu chochote kinachotokea kwake au Ery Kingu uwa wanaambia ndio maana ilikuwa rahisi kwake kujua.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.