“Mitandao Ya Kijamii Inavuruga Wasanii”- MB Dogg

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva ambaye anahusika kwa kutengeneza vibao vikali kama vile ‘Latifah’ na ‘Ina Maana’ Mbwana Mohamed ‘Mb Dogg’ amefunguka na kuitupia lawama mitandao ya kijamii na kudai ndio imesababisha wasanii kuharibikiwa.

MB Dogg amefunguka hayo alpokuwa anaongelea baadhi ya matukio ambayo yamewakumba wasanii kadhaa kama Wema Sepetu na Amber Rutty wanaodaiwa kusambaza video zao chafu kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mb Dogg alisema anashukuru viongozi wamekuwa macho na kuchukua hatua lakini anachukia mitandao kwani imefanya watu wengi kuiga kwa kila wanachokiona.

Sisi watu weusi tuna njia zetu za kuishi sasa mitandao imetuletea ugeni na sisi hatuwezi kutumia, tukiona mtu fulani kafanya hivi basi tunaiga.

Basata watoe misingi vizuri, walianza na video ambazo zamani ilikuwa mguu ukionekana sawa lakini ukizidisha inawekwa kapuni, wakikaza kwa kutoa elimu kwa wasanii zaidi tunaweza kukaa kwenye laini vizuri na matukio kama haya yasitokee tena.”

Wema Sepetu na Amber Rutty wameshachuliwa hatua za kisheria kwani kila mmoja amekwisha fikishwa mahakamani na kesi zao tayari zinashughulikiwa.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.