Loading...

Mke wa Mzee Yusuf adai anataka kuacha muziki, hii ndio sababu yake

May 18, 2017 at 17:52
Mzee Yusuf na mkewe, Leyla Rashid

Leyla Rashid ambaye ni mke wa Mzee Yusuf na muimbaji wa kundi la Jahazi Modern Taarab amedai kuwa anatamani kuacha muziki kama mume wake ili kumtumikia mungu.

Msanii huyu wa nyimbo za Taarab aliyasema haya katika mazungumzo na Showbiz Xtra aliposema kuwa anatamani sasa kumuunga mume wake na ndio maana anafikira za kuacha kuimba nyimbo hizi. Leyla alisema,

Mzee Yusuf na mkewe, Leyla Rashid

Mzee Yusuf na mkewe, Leyla Rashid

“Ukweli naimba tu lakini sina munkari kama zamani hasa baada ya mume wangu kujitoa kwenye kundi na kumrudia muumba, sijaacha rasmi kuimba ila nafikiria zaidi kumfuata mume wangu katika kumtumika Mwenyezi Mungu,” alisema.

Mzee Yusuf atahivyo hana shida na mke wake kuimba lakini iwapo anataka kuacha kuimba basi hana budi bali kumuunga mkono

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on social pages by clicking on them below