Mo-Jay Akiri Kumpiga Gigy Money Akiwa Kwenye Hali ya Ujauzito.

Siku za nyuma hivi  msanii wa kike bongo Gigy Money, aliandika post kubwa katika ukurasa wake wa instagram huku akilalamika kuwa mwanaume aliyempa ujauzito amekuwa akimtesa na kumpiga .Gigy alilalamika na kusema kuwa mwanaume huyo amekuwa hajali sana hali yake ya ujauzito na kumpiga sana akiwa katika hali kama ile.

Hata hivyo wakizungumza walipokuwa pamoja katika red kapeti ya usiku wa Nandy,Aslay na marafiki , Gigy Money alianza kwa kusema kuwa walishayazungumza mambo hayo na sasa hivi wako sawa kabisa ingawa mara nyingi amekuwa akimshatika mpenzi wake huyo kwa wazazi wake lakini siku hiyo ilikuwa ni too much ndio maana aliamua kumpost instagram kwa sababu anajua kabisa kuwa mpenzi wake sio mtu wa  kupenda kuwekwa katika mitandao.

download latest music    

Ilikuwa ni lazima tupatane  ndio maana sikumponda wala kumtukana lakini niliandika na kuongea kwa wote  sio mo pekee yake huwa nakosega kuna muda mwanaume anakuwa na hasira moaka anaamua kumpiga mwanamke wake.lakini ameniomba msamaha na yameisha ingawa mara nyingi nikiwa na hasira huw aninamwambia mama yake au mama yangu lakini siku ile ilikuwa too much.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo za kumpiga mzazi mwenzie Mo-jay alikiri kuwa ni kweli alimpiga lakini sio kipigo kikubwa kama wanavyodhani na hiyo yote ilisababishwa na hasira za Gigy Money mwenyewe.

Unajua wakina mama wanapokuwa katika hali aliyonayo gigy wanakuwa ni vigumu sana kuwaelewa,unaweza ukafanya kitu kidogo yeye akachukulia kuwa ni kikubwa na honestry kuna kitu alikiwa amefanya ambacho kilikuwa kinahatarisha maisha ya mtoto hivyo  na alinikera na sio mara moja mara mbili amekuwa akikifanya kwaiyo sikumpiga insuch lakini hakikuwa sawa kwaio nilipata hasira kama mzazi na tukakwazana nae na kwa sababu yuko kwenye hali kama ile anakuwa anafikiria mengi sana.

lakini sio kipigo ambacho watu wanasema nimempiga lakini ni ile tu kukwazana na kurekebishana na ndio maana hata mkikwazana na akigeuka mara moja mara mbili hakuoni wala haupigi simu basi anakuwa anapata hasira sana.

Hata hivyo Gigy Money na mzazi mwenzie Mo-Jay wanasema wanategemea kupata mtoto wa kike na tayari walishapata jina la kumwita atakuwa akiitwa Candy ambapo wanategemea kuanzia mwezi ujao siku yoyote wanatarajia kupokea mtoto wao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.