Loading...

Monalisa Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Uganda

November 09, 2018 at 07:32
Monalisa Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Uganda

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu Kama Monalisa amepata tuzo nyingine kutoka nchini Uganda Kupitia Sanaa yake ya maigizo.

Monalisa amejipatia Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.

Loading...

Baada ya kutangazwa kupata tuzo hiyo jana tarehe 08/11/2018 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.

Bi. Fissoo ametoa pongezi hizo ofisini kwake ambapo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako”.

Lakini pia Monalisa alifunguka Baada ya kupokea salamu hizo za pongezi kutoka kwa Bifu ya Fulani Tanzania:

Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha”.

 

Share

Comments

  1. congratulations

  2. vyema

  3. congratulations

  4. hongera mami

  5. asante Sana kwa kutuwakilisha sisi Watanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…