Moni Amkana Roma Mkatoriki,Asema Hana Mchango Wowote kwake.

Msanii wa musiki wa Hip-Hop nchini Moni Centrozone amefunga na kusema kuwa msanii mwenzie Roma hana mchango wowte katika musiki wake kama watu wanavyokuwa wanafikiria.Moni amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakisema kuwa amekuwa msaada mkubwa katika muziki wake lakini ukweli ni kwamba hakuna chochote zaii ya kumpa shida tu tena hasa baada ya kutoa nae wimbo ambao wengi walihisi utasaidia kumtambulisha lakini imezidi kumletea shida.

Moni alitoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusu kuunganika kwao na Country Boy na kuleta muungano uliojulikana kama MoCo ili kuweza kushindana na muungano wa Rostam ambao ni muunganiko wa Roma na Stamina, ndipo aliposema kuwa kwa upande wake hana mashindano na mtu yoyote zaidi ya kufanya muziki wake.

download latest music    

Moni anasema kuwa katika watu ambao hawezi kuwasahahu katika muziki ni marehemu Langa ambae alikuwa  wa kwanza kugundua kipaji chake tangu zamani na kuweza kumsadia kumpa njia kuingia katika muziki.

Who is Roma kwenye maisha yangu,mimi simfahamu na wala hajawahi kunitoa katika muziki kama watu wanavyodhani.namjua langa ambae alinitoa uswahili na kunileta mjini.sipeni kutajiwa majina ya watu wasiokuwa na umuhimu katika maisha yangu.

Moni ameendelea kusema kuwa kundi alilolianzisha na Country haliwazuhii kufanya muziki wao kama solo artist ,lengo la kundi ni kuleta changamoto kwa wasanii wengine.

Moni na Roma walishawahi kufanya kazi ya pamoja na kumfanya Moni kujulikana sana , ambapo ukaribu wao ulipelekea wawili hao kutekwa mnamo April mwaka huohuo.Baada ya kuachiwa kutoka kusikojulina msanii Roma alitoa wimbo ulijulikana kama Zimbabwe ambao ulielezea kwa ufupi tukio ilo lakini kumbe Moni alichukia  kitendo icho na kusema kuwa Roma ametumia idea ya kutekwa kama tukio ilo lilimpata peke yake ilhali walikuwa wanne.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.