Mr. Liquid Awatuhumu Rayvanny na Diamond

Moja ya watu maarufu sasa hivi katika mitandao ya kijamii anaejulikana kama Mr Liquid amefunguka na kutupia lawama zake kwa wasanii wawili Daimond na Rayvanny kwa kusema kuwa wasanii hawa wanatumia kionjo chake kwa ajili ya kujinufaisha bila kuwa na makubaliano.

Mr Liquid anasema kuwa wasanii hao wamekuwa wakijinufaisha na kionjo icho bila kuwa na ruhusa yake wakati yeye ndio alitakiwa kuwa na makubaliano na wasanii hawa kabla ya kutumia kionjo icho.

download latest music    

Tetema ndio wimbo na kionjo changu maarufu sana , wanatumia kionjo changu kupiga pesa bila kuwasiliana na mimi.

Ukiachana na misuko suko wanayopitai wasanii hawa hasa kila mara wanapotoa wimbo kwa kuambiwa wanakopi au kuiba vionjo au kufungiwa na mamlaka husika lakini wasanii hawa wamekuwa wakifanya kazi za pamoja na kufanikiwa sana kila mara.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.