Loading...

Mr. Nice Amjia Juu Young Dee Baada ya Kuimuibia Wimbo Wake Wa ‘King’asti’

December 07, 2017 at 07:42
Mr. Nice Amjia Juu Young Dee Baada ya Kuimuibia Wimbo Wake Wa 'King'asti'

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyetamba kwa staili yake ya ‘Takeu style’ ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Young Dee baada ya kusample wimbo wake wa ‘King’asti’.

Mr. Nice amezidi kukaa kwenye headlines kwa wiki hii kuanzia kurudi upya kwa bifu lake na aliyekuwa hasimu wake mkubwa Dudubaya mpaka kuingia kwenye vita ya maneno na Paka rapa Young Dee baada ya Young Dee ku-sample wimbo wake ulio-hit miaka ya nyuma ulioenda kwa jina la ‘king’asti’.

Loading...

Young Dee ametoa wimbo wake mpya unaoitwa ‘kiben-10’ na amemshirikisha Dayna Nyange ambapo kwenye wimbo huo kuna kionjo na mashairi machache kutoka kwenye wimbo huo wa Mr. Nice ambao amechukua bila ruhusa ya mwenye wimbo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr. Nice amemtolea Young Dee povu zito:

Nadhani ni wizi na ni aibu kuchukua kazi ya mtu na kuirudia tena kwa manufaa yako binafsi bila hata kuomba ridhaa yoyote kutoka kwa mwenye kazi yake, ni wizi ambao serikali na jamii nzima imekuwa ikipiga vita every day na ni kosa kubwa kabisa kisheria…..Huyo msanii anayeitwa sijui Young Dee mwelezeni asije kutafuta huruma yangu hapo baadae kwa maana haitakuwepo”.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.