Mr.Touch Amchokoza Tena Nay, Amkwapua Moja ya Wasanii wake

Aliyewahi kuwa mtayarishaji katika studio ya Free Nation Mr.T-touch amejitayarisha kuingia tena katika vita na msanii Nay wa Mitego baada ya kumchukua msanii Bgway  na kumtambulisha kama msanii wake mpya ambae yuko chini yake.

Msanii huyo ambae alishawahi kuimba wimbo na nay wa mitego unaojulikana kama sijachukia, sasa hivi yuko chini ya Mr.T-Touch baada ya kutoka kwa Nay wa mitego, hata hivyo msanii huyo alisikia akisema kuwa tangu ameazna kukaa na nay na kufanya nae kazi hajwahi kutumia hata elfu 2 yake na anashangaa alikuwa akim-menage nini.

download latest music    

Huyu mimi nimshikaji wangu befor hata nay, yaani nilianza kumjua huyo kala ya nay, na swala la mimi kufanya kazi na huyo ni swala ambalo lilikuwepo tu siku nyingi hata kama asingeenda kwa nay , ilikuwa ni lazima ningefanya nae kazi tu.

mimi na yeye tuko kwa ajili ya kazi tu na mimi sio meneja wa bgway ila mimi na yeye tunafanya kazi pamoja chini ya Isbar, na kwasabau huyu mimi ni rafiki yangu tangu zamani tangu naondoka kwa ney nilikuwa namwambia njoo tufanye kazi wote.

Alipotafutwa Ney wa mitego kuelezea amepokeaje maamuzi ya bgway na t-touch kufanya kazi pamoja alisema kwa sasa amesafiri kikazi lakini atakaporudi ataweka mambo sawa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.