Msami Ajuta Kutembea Na Uwoya,Alishawahi Kukutana Na Ndikumana.

Msami ni mmoja wa wasanii wa bongo fleva wanaofanya vizuri katika kuimba na kucheza pia,lakini pia msami ni moja ya wanaume wanaosemekana kuwa na uhusiano na Irene Uwoya kipindi ambacho Irene alikwa tayari ameshafunga ndoa na Ndikumana.

Akiongea na mwandishi kutoka Millard ayo, Msami anakiri kuwa alikuwa na uhusiano na Irene Uwoya lakini alipouliza mahusiano hayo alimbiwa kuwa wameshagombana, lakini baaada ya kufatilia sana alikuja kuona kuwa wawili hao hata kama wamegombana lakini bado wapo katika ndoa na kwa maadili ya dini ya kikristo ndoa hiyo haijavunjika.

download latest music    

Lakini pia Msami anasema kuwa hata baada ya kugundua kitu hicho aliongea na Irene na kumuomba waachane ili awe huru kwa sababu nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa kitendo hicho cha kutembea na mke wa mtu.

Msami anasema kuwa alishawahi kukutana na Ndikumana mara moja uwanja wa ndege, na hakuwahi kuwa na bifu nae na hata alipopata taarifa za msiba aliumia sana na kuonyesha hisia zake alimpigia Irene Uwoya na kumpa pole ingawa hawakuweza kuelewana vizuri sana hivyo pia aliamua kumpost Ndikumana instagram aktika ukurasa wake kama njia ya kuonyesha kuguswa kwake.

Katika kuongezea kwake ,Msami anasema kuwa hawezi kujua mpaka Ndikumana anafariki alikuwa anawaza nini kuhusu yeye lakini anachoamini kuwa yeye aliongea na mungu wake kuhusu dhambi aliyotenda ya kutembea na mke wa mtu na anaamini atasameheka.Akiendelea kwa kutoa ushauri Msami anasema kuwa kwa kipindi hiki kigumu Irene anachopitia inabidi awe mvumilivu na wala hasiskilize maneno ya watu, lakini aangalie jinsi ya kumlea mtoto wake wa kiume aliempata na Ndikumana na kumpa malezi bora maana maneno katika mitandao huwa yanaishi hivyo mwanae atayakuta.

Mimi na Ndikumana tulishakuta mara moja airport alikuja kutupokea,na tulisalimia vizuri tu na kitu kikubwa watu wanatakiwa kujua upaswi kumpenda mtu akiwa amekufa au amepata matatizo , nilifurahi kwa kile alichokifanya Hamisa kwa Lulu.

Nilikuwa naheshimu sana ndoa ya Irene na Hamad, na nilikuja kujua nimefanya makosa kutembea na Irene, na sababu kubwa ya kuachana na Irene ni baada ya kugundua kuwa ni makosa kutembea na mtu aliyefunga ndoa na bado hajaachana na mumuwe, hivyo nilimwambia Irene ni bora tuachane.Mimi ni mkristo na dini yetu hairuhusu hivyo

Kwa Irene wapo watakao mbeza na wapo watakao mfariji hivyo azingatie wale watakao mtia moyo tu kwa kipndi hiki, na kujua ni jinsi gani ya kumlea mwanae maana maneno ya mitandao yapo na atakuwa atayakuta. -Alimalizia Msami

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.