Msanii Wyse Amtetea Ben Pol Dhidi Ya Tetesi Za Kuwa ‘Kibenteni’

Msanii wa muziki wa Bongo fleva maarufu kama Wyse ambaye Hivi sasa anatamba na single yake ya ‘Chota’ Ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Ben Pol.

Ben Pol amekuwa akitengeneza headlines na Mpenzi Wake Mpya Anerlisa ambapo mrembo huyo anatajwa kutokea kwenye Familia yenye mkwanja mrefu kiasi ya kwamba inasemekana Hivi sasa anamlea Ben Pol.

download latest music    

Msanii Wyse ameibuka na kukataa kabisa taarifa na hizo na kusema wazi kuw Ben Pol sio kibenteni na wala hayupo na mwanamke Yule kwa ajili ya pesa kama wengi wanavyodhani bali ni mapenzi ya dhati kwani tayari Ben Pol ana pesa zake binafsi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Wyse amefunguka haya kuhusu mahusiano ya Ben Pol na Mpenzi Wake Anerlisa:

Ben Pol pia ana mkwanja mrefu pia yaani kwa kifupi ni kwamba pale hakuna mtu ambaye anamlea mwenzake, ni watu ambao wameridhiana”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.