Loading...

Msiba Watengeneza Bifu Zito Kati Ya Isabela na Baby Madaha

February 11, 2019 at 09:01
Msiba Watengeneza Bifu Zito Kati Ya Isabela na Baby Madaha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Baby Madaha na msanii mwenzake wa Bongo movie Isabela wamedaiwa kuwa kwenye Bifu zito na kisa kinatajwa ni msiba.

Global Publishers wanaripoti kuwa wawili hao ambao walikuwa marafiki walioshibana kwa sasa wamekuwa maadui chanzo kikitajwa ni Baby Madaha kutohudhuria mazishi ya dada wa Isabela ambaye alifariki dunia hivi karibuni.

Loading...

Katika mahojiano na GPL,  Isabela aliulizwa  kuhusiana na hilo alisema ni kweli hampendi Baby Madaha na urafiki wao umeshavunjika kwani alishindwa kumpa ushirikiano alipofiwa na dada yake jambo ambalo linamuumiza mpaka sasa.

Kitendo cha kutokuja kwenye msiba wa dada yangu kiliniuma sana na mpaka sasa naumia maana Baby Madaha ni rafiki yangu wa damu, aliniachia msiba nizike peke yangu na anajua fika kwamba yeye ndiye rafiki yangu mkubwa nimekasirika sana huo ndiyo ukweli“.

Lakini Baby madaha amesema kuwa hana Bifu na Isabela na yeye mwenyewe anajua kwanini hakuhudhuria mazishi ya dada yake kwani alikuwa nje ya nchi.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…