Mtoto Wangu Amebadilisha Maisha Yangu- Irene Paul

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Paul amefunguka na kuweka wazi Jinsi Mtoto Wake wa kwanza alivyoweza kubadilisha maisha yake na kumpa Furaha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti pa Ijumaa, Irene Paul amefunguka na kuweka wazi Jinsi binti yake anayeitwa Wendo alivyoweza Kumbadilisha kabisa maisha yake:

download latest music    

Kuna vitu vingi sana, yaani sijui nisemeje lakini kifupi maisha yangu yote yamebadilika kwani kuwa mama ni kitu kingine tofauti na usichana”.

Irene ameweka wazi kutokana na Upendo alionao kwa mwanaye hajawahi muacha na Dada wa kazi kabisa:

Kwanza unavyoniona mimi toka mwanzo sikupenda mwanangu akae nyumbani na dada wa kazi, nilitaka kumuangalia mwanangu hatua kwa hatua, hata mama yangu mwenyewe alinishangaa na ndivyo hivyo nikiwa na kazi zangu anakuwepo mama yangu au ndugu yangu“.

Lakini pia Irene ameweka wazi mipango yake ya kuongeza mtoto mwingine katika siku zijazo.

Ndio, nina mpango huo kwani kama unavyoona nina mmoja tu, Mungu akinibariki mwingine nitashukuru”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.