Loading…

Muda Wa Kanumba Kuondoka Duniani Ulikuwa Umefika- Shamsa Ford

November 14, 2017 at 13:43
Muda Wa Kanumba Kuondoka Duniani Ulikuwa Umefika- Shamsa Ford

Msanii wa filamu za Bongo fleva, Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa muda wa Kanumba kuishi duniani ulikuwa umefika ndio maana akatangulia mbele ya haki kwa wakati ule.

Siku ya Jana Elizabeth Michael almaarufu kwa jina lake la uigizaji kama Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika mahakama kuu ya Tanzania baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukisudia mpenzi wake na muigizaji mwenzake Steven Kanumba miaka mitano iliyopita.

Loading...

Baada ya hukumu hiyo kutolewa watu mbalimbali wakiwemo mastaa wamejitokeza kutoa michango yao ya hali na mali huku kila mmoja akionekana kusikitishwa na kitendo hiko.

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford pia amefunguka kwenye mahojiano na Millard Ayo na kueleza yaliyo moyoni mwake na kusisitiza kuwa Kanumba  alipoteza maisha ile siku kwa sababu ilikuwa imeshaandikwa iwe hivyo.

Kusema ukweli baada ya kusikia Lulu amefungwa miaka miwili jela nilijisikia vibaya sana kwa sababu naamini atakuwa katika wakati mgumu sana huko alipo lakini mwisho wa ukiangalia kila linalotokea kwa mwanadamu basi ujue mwanyezi Mungu amelipanga kwaiyo kuna njia sahihi ambayo Mungu anampeleka na ndio maana anampitisha kote huko kwa cha msingi kwake ni kuwa jasiri lakini kiukweli nilimuonea huruma sana ukiangalia yule bado ni biinti mdogo sana mwenye ndoto nyingi na ukiangalia muda katika maisha ni kila kitu”.

Lakini pia Shamsa alimuongelea Kanumba ambaye anaaminika kuwa ameacha pengo kubwa sana katika tasnia hii ya filamu na kudai kuwa anaamini kuwa Kanumba alikufa siku ile kwa sababu siku yake ilikuwa imefika kwaiyo watu wasipende sana kumuhukumu mtu kilichobaki ni kumuombea tu mwenzetu ambaye tuko naye duniani.

 

 

Comments

  1. Ila tufanyeje na uamuzi umeshatolewa

  2. Ni kweli kabisa

  3. Basi kesi imekwenda hivo

  4. Mpango wa muumba hauwezi kubadilika

  5. Ilikua iwe hivo tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.