Muigizaji Mtoto wa Miaka Minne Amlilia Mzee Majuto

Mtoto wa miaka minne ambaye anakuja kwa kasik katika tasnia ya uigizaji na Uchekeshaji Maisara Mohamed maarufu kama Maizumo amefunguka kusikitishwa na Kifo cha Mzee Majuto.

Mtoto huyo ameweka wazi kuwa ndoto yake kub a ilikuwa ni kuigiza na Marehemu Mzee Majuto aliyeaga dunia siku chache zilizopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, mtoto huyo amefunguka kuwa alikuwa anampenda sana King Majuto na alimuomba baba yake amkutanishe naye lakini hakufanya hivyo.

Nilikuwa nampenda sana King Majuto, nilikuwa napenda kuangalia muvi zake pamoja na matangazo yake, baba aliniambia atanipeleka nikamuone lakini hatukwenda mpaka amekufa”.

Baba Mzazi wa Maizumo Mohammed Omary ambapo kwa upande wake alisema kuwa siku ya msiba unatokea hakuwa nyumbani lakini aliporudi alimuita Mai nakumwambia kuwa Majuto amefariki lakini chakushangaza alilia sana kama mtu mzima na hata shuleni alikuwa anakataa kwenda, hivyo wakafanya kumlazimisha.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.