Mume wa Mama Diamond Kwenye Skendo Nzito na Mke Wa Mtu

Maisala Shante ambaye ni Mume halali wa Mama mzazi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi Sandrah amejikuta katika skendo nzito na Mke wa mtu.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wamenasa SMS za Shamte ambazo alikuwa anachati na mwanamke ambaye anaaminika kuwa mke wa mtu na kuibua maswali juu ya ukaribu wao ilhali wote wapo kwenye ndoa.

download latest music    

Mwanamke ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu alikuwa anachat kimahaba Lakini pia inadaiwa Kwenye meseji hizo walikuwa wanatumiana picha kudhihirisha mambo yamekolea.

Gazeti la Risasi lilimsaka Mwanamke huyo ambaye alikataa kabisa tetesi za Mahusiano na Shamte na kufunguka haya:

Nimekuambia simu yangu ilipotea, unachoniambia mimi sikikumbuki kabisa kama niliwahi kuchati na huyo mwanaume chochote, lakini pia kama nitakuwa nimechati naye kuna ubaya gani, si mwanaume kama wanaume wengine“.

Baada ya mwanamke huyo kubanwa na kufunguka hayo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Shamte ambaye alidai kuwa hana tabia za kuchati na wanawake.

Nakuheshimu kama mwandishi kukujibu swali hili, mimi sijawahi kuchati na wanawake ovyo, kama una namba ya huyo mwanamke nitumie ndio nitakujibu“.

Shamte ni mume halali wa Mama Diamond, walifunga ndoa mwaka jana na baada ya ndoa hiyo kukazuka ‘vijineno’ ikiwemo madai kuwa mwanaume huyo ni marioo na ndoa yao haitadumu. Hata hivyo, wawili hao wameendelea kuwa pamoja na kuwafanya watu waamini kwamba, kweli mapenzi hayachagui umri, kikubwa ni kuwepo kwa mapenzi ya kweli.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.