“Mume Wangu Ameniingiza Kwenye Bongo Fleva”-Riyama Ally

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie Riyama Ally amefunguka na kuwekan wazi kuwa mume wake ambaye ni msanii wa Bongo fleva Hajji Mwalimu maarufu kama Leo Mysterio ndiye aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa Bongo fleva.

Siku za hivi karibuni sauti ya Riyama Ally imesikika katika moja ya nyimbo mpya za Leo Mysterio unaoitwa Wanaume wa Dar na mara moja Riyama ameweka bayana kuwa pamoja na kuwa hana kipaji cha kuimba lakini mumewe alivyomuomba ilibidi akubali.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Riyama amesema kuwa, yeye si muimbaji kivile lakini linapokuja suala la kumsapoti mume wake, haoni shida kujiingiza huko.

Sina kipaji cha kuimba, napenda sana kuigiza ila nitakuwa namsapoti mista wangu katika nyimbo zake kama vile kuingiza maneno kuntu”.

Lakini pia Riyama ameweka wazi kuwa wimbo huo umetungwa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha wanaume wasiopenda kufanya kazi na kukaa vijiweni kuinuka na kuacha kuchagua kazi wakati wanategemewa.

Kama ni kijana akisikiliza wimbo huo ambao nami nimeimba, atapata fursa ya kujifunza jambo”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.