Loading...

Muna Ahaidi Kufunga Mpaka Hukumu Ya Lulu Itakapokwisha

November 17, 2017 at 09:47
Muna Ahaidi Kufunga Mpaka Hukumu Ya Lulu Itakapokwisha

Muna , akiwa ni kama ndugu kwa Lulu Michael alijitolea kwa hiari yake kuwa dada wa hiari wa Lulu tangu kipindi wanaigiza wote kipindi wapo kaole sanaa group,  Muna amekuwa karibu na familia ya Lulu kwa kipidi chote cha raha na shida na sana sana   katika kipindi hiki cha miwsho cha kesi ya Lulu mpaka anapata hukumu yake. Pamoja na kwamba Muna  alikiri kuwa alikuwa na mgonjwa hospitali lakini bado Muna aliweza kuhudhuria katika kesi hiyo  kila siku ili kumfariji mdogo wake huyo.

Akiongea na waandishi wa habari, Muna alielezea jinsi ambavyo ameipokea hukumu ya mdogo wake Lulu kwa masikitiko ukizingatia ndie ndugu na rafiki wa karibu aliekuwa nae kwa kipindi kirefu na tangu wajuane hawajawahi kugombana,lakini pia Muna bado anajipa moyo na kusema kuwa hukumu ya miaka miwili kwa Lulu ni moja ya jaribu tu ambalo Mungu ameamua kumpitisha Lulu huku akimundalia mema zaidi mbele ya safari yake.

Loading...

Unajua mimi namuamini sana mungu na ninaamini ilo  ni moja ya jaribu tu  ambalo Mungu ameamua kumpa Lulu lakini ipo siku litapita tu na lulu atarudi katika maisha yake ya zamani.-Aliongea Muna kwa kujipa matumaini makubwa

Lulu na Muna katika picha za pamoja

Hata hivyo kwa masikitiko makubwa kabisa Muna anasema kuwa atakumbuka sana kipindi amvacho alikuwa na Lulu,na kufanya mambo mengi kwa pamoja kwa shida na raha lakini leo anafanya peke yake, mbali na hayo muna amehaidi kufunga kwa sala kwa siku zote ambazo Lulu atakuwa hukumni ili kumuombea.

Nitakumbuka nyakati zote nilizokuwa na yeye kipindi yupo uraiani,lakini kuanzia siku aliyopewa hukumu kazi yangu ni moja tu  kufunga na kuomba kwa ajili yake.-Alimalizia Muna

Wapo wengi walionekana kuguswa na hukumu ya Lulu lakini pia Muna akiwa kama mwanafamilia na rafiki wa karibu wa Lulu Michael anaamini kuwa ndugu yake huyo anahitaji maombi ya muda mrefu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazomkabili kipindi atakapokuwa gerezani ukizingatia wengi waliotoka huku wamekuwa wakielezea ugumu wa maisha ya kutokuwa huru.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.