Muziki Wa Dansi Haujafanya Vizuri Mwaka 2017 Kwasababu Umefunikwa na Bongo Fleva- Christian Bella

December 15, 2017 at 11:07
Muziki Wa Dansi Haujafanya Vizuri Mwaka 2017 Kwasababu Umefunikwa na Bongo Fleva- Christian Bella

Mkali wa muziki wa Dansi nchini Christian Bella Obama ameibuja na kudai kuwa muziki wa  dansi haukufanya vuzuri kabisa kwa mwaka huu wa 2017 kwa saabu mziki wa Bongo fleva umeuzima kabisa.

Christian Bella sio msanii wa kwanza kulalamika kuwa mziki wa aina nyingine zaidi ya Bongo fleva haukufanya vizuri ni siku chache tu zilizopita mkali wa mziki wa Taarabu nchini Khadija Kopa alidai kuwa mziki wa Taarab haukufanya vizuri kwa mwaka huu kwa sababu ya sheria ya Makonda ya mziki mwisho saa sita.

Loading...

Lakini pia msanii wa Hip hop Kala Jeremiah amekiri kuwa mwaka 2017 haukuwa mwaka mzuri kwa mziki wa hip hop kwani haukuvuma kabisa, pia Msaga Sugu mkali wa Singeli alikiri pia mziki huo ulidoda kwa mwaka huu wa 2017.

Christian Bella aliongelea mziki wa Dansi ambao hufanya vizuri kila msimu lakini amedai kwa mwaka huu umedoda kwa sababu ya nafasi kubwa ya mashabiki wameegemea zaidi kwenye mziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliofanya na East Africa TV Bella amekiri pia sababu nyingine iliyozima mziki wa dansi kwa mwaka huu ni wasanii wa dansi kutopendana.

Dansi haijafanya vizuri na sio kwamba wasanii hawapo ila nahisi ni upepo tu haujakaa vizuri tujitahidi tu kujituma lakini mara nyingi kwenye kundi la watu kumi ishirini kuna kuchukiana na ninasema hivyo kwa sababu nimetokea kwenye kundi chuki za kuchekeana machoni Lakini moyoni tumejaza chuki”.

Kuna watu wengi waliongelea suala la ushindani na bifu la Diamond na Alikiba kuwa limetawala sekta ya muziki na sio tu limezima a in a nyingine ya miziki kusikiliza bali hata hump hump kwenye Bongo flea kuna wasanii hawasikiki kwasababu ya ushindani wa Diamond na Alikiba.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.