Mwaka 2019 Lazima Niolewe Nimechoka Kusubiri- Tiko

Muigizaji wa Bongo movie na msanii wa Bongo fleva Tiko Hassan ameibuka na kuweka wazi nia yake kutaka kutafuta mume na kuolewa kwa mwaka huu wa 2019.

Tiko amefunguka na kusema yeye Kama mwanamke ambaye anajiamini kuwa amekamilika anatamani sana apate mwanaume wa kuwa mwenza wake kwani amechoka kusubiri.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Tiko alisema kuwa ndoa ni heshima kwa kila mwanamke na amesubiri kwa muda mrefu bila mafanikio lakini imani yake ni kwamba, atauona mwaka wa 2020 akiwa ni mke wa mtu.

Jamani nimechoka kusubiri lakini naamini mwaka huu utakuwa ni mzuri kwangu, kila kwenye ibada namuomba Mungu anijaalie mume bora ndani ya mwaka huu“.

Lakini pia Tiko ameweka waiz anataka mwanaume ambaye atakuwa na utayari wa kumuelewa kutokana na kazi anayofanya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.