Mwanaheri Ampongeza Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo.

Mwanamaigizo anaefanya vizuri katika tasnia na kazi yake Mwanaheri amefunguka na kumpongeza sana Naibu Waziri wa Sanaa , Habari na Michezo Mh .Juliana Shonza kwa kitendo chake cha kuwafungia na kupiga marufuku uvaaji wa nguo mbaya katika kazi za sanaa kwa wasanii wote wa maigizo na muziki kwa sababu zinavunja maadili ya Tanzania.

Mwanaheri anasema kuwa kitendo cha Naibu waziri kukataza uvaaji wa nguo chafu utasaidia kurudisha hadhi ya sinema za bongo movies nchini kwa sababu wasichana wengi walikuwa wakikosea sana kufanya hivyo.Mwanaheri anasema kuwa wasichana ho wamekuwa wakishusha hadhi ya bongo movies kwa sababu wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo na kusababisha watu wengi kutopenda kuangalia movie zao, hivyo anamshukuru sana Mh Naibu waziri.

download latest music    

Sijawahi kuvaa nusu utupu, na wala sidhani kama itatokea,ninaipongeza sana serikali kwa kitendo chake cha kukataza mavazi kama hayo na picha za nusu utupu zilizokuwa zikiwekwa katika mitandao na wasanii kwa sababu kwanza zinaharibu maadili ya kitanzania,ninachoamini kupitia ili hadhi ya bongo movies na filamu itarudi kwa sababu jaii ilitudharau kutokana na mambo hayo.

Hivi karibu kuna baadhi ya wasanii wamepata adhabu baada ya kuwa na tabia ya kuvaa na kuweka picha za utupu katika mitandao ikiwa ni moja kati ya hatua kubwa zinazofanywa na serikali kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa maadili unaofanya na wasanii ambao wamepewa dhamana ya kuwa vioo katika jamii tunazoishi.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.