Mwanamuziki wa Kenya Bahati aelezea masaibu aliyopitia chini Lulu Michael

Mwanamuziki wa Kenya Bahati wakati huu ako Tanzania kwenye tour yake ya wimbo wake na Ray Vanny ambao uliachiliwa juzi na ambao unapatikana wasafi.com.

Katika pilka pilka hizo alijipata kwenye Magic FM ambapo alizungumzia mambo mbali mbali ikiwemo Lulu Michael na vile alipomhangaisha.

download latest music    

Kwa wote wanaojua msanii huyo, amekuwa akizunguliwa na Lulu Michael kwa muda mrefu na kwa hio alitaka akue kwenye video yake ya Maria.

Alikuja hadi Dar kumfata Lulu lakini hakufanikiwa.

Hii ni siri ambayo nadhani hata Wakenya hawakujua, AY peke yake ndiye alijua. Nilitoka Nairobi kuja hapa [Dar es Salaam] natafuta connection na Lulu kwasababu nataka awe kwenye ile video [Maria] ambayo nimemweka Jokate. Nimekaa kwa hotel Lulu amekataa kushika simu mpaka ikafika mahali nikamwambia ukija kuniona Mungu atakubariki, siku ya pili akakataa kabisa nikamwambia mshikaji AY acha tu nirudi nyumbani. Nikarudi hivyo,” Alieleza.

Bahati ameongeza kuwa sababu ya kufanya kazi na Ray Vanny katika wimbo wao mpya ‘Nikumbushe’ ilikuwa ni mipango yake ya muda mrefu ili muziki wake uweze kupata tobo hapa nchini.

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi